Powered By Blogger

11.12.17

Je! Ulikikosa kikombe cha babu wa loliondo ni zamu yako sasa kikombe kinapatika kwa babu

        dulahots.blogspot. com
Ngorongoro. Mchungaji Ambilikile Mwasapile maarufu Babu wa Loliondo aliyehudumia maelfu ya watu ndani na nje ya nchi kwa dawa aliyoitoa kwa kipimo cha kikombe amedai ameoteshwa kuwa umati utarudi kijijini Samunge kupata dawa. 

Amesema ana uhakika wa jambo hilo kwa kuwa hata mwaka 2011 kabla ya maelfu ya watu kufika nyumbani kwake alioteshwa, hivyo amejiandaa kuweka miundombinu bora zaidi na hasa ujenzi wa vibanda atakavyovitumia kutoa huduma. 

Mchungaji Mwasapile alisema hayo jana Jumapili Desemba 10,2017 mbele ya ujumbe wa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Joseph Kakunda aliyekuwa mkoani Arusha kukagua miradi ya maendeleo, ikiwemo ya kuwawezesha wananchi kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi. 

Miongoni mwa waliofika kupata ‘kikombe’ kwa gharama ya Sh500 mwaka 2011 walikuwemo wafanyabiashara maarufu, wanasiasa na viongozi waandamizi serikalini. 

Akizungumzia dawa yake anayodai inatibu maradhi mengi amesema kwa sasa anaitoa kwa watu wachache wanaofika kijijini hapo. 

Miongoni mwao amesema ni watalii wanaofika kutembelea vivutio vya kitalii vilivyopo katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. 

"Huwa nawauliza watalii namna walivyoifahamu dawa yangu wanasema habari za ‘kikombe cha Babu’ imeenea katika nchi zao za Ulaya na Amerika," amesema Mwasapile. 

Naibu Waziri wa Tamisemi, Kakunda akiwa na ujumbe wake baada ya kupata kikombe alimshukuru Mchungaji Mwasapile kwa alivyolifanya Taifa kujulikana na kusababisha maendeleo ya kijamii katika Kijiji cha Samunge. 

Ametoa mfano wa barabara ya kutoka wilayani Longido na Kigongoni wilayani Monduli ambazo zimeboreshwa kutokana na idadi kubwa ya watu waliokuwa wakifika kupata huduma ya dawa. 

Amesema hata huduma ya mitandao ya mawasiliano ya simu ilifika eneo hilo kwa haraka kutoka na watu wengi waliohitaji kuwasiliana na ndugu zao. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Raphael Siumbu amesema Mwasapile amechangia shughuli za maendeleo kutokana na idadi kubwa ya waliokwenda kijijini hapo na kusababisha mzunguko wa fedha kuwa mkubwa. 

Amesema watu wengi kijijini Samunge  wamepanda miti inayotumika kutengenezea dawa hivyo kuchangia utunzaji wa mazingira na huduma za kijamii kuongezeka.

Mohammed salah ashinda tuzo ya mchezaji bora afrika mwaka huu

Www.dulahots.blogspot.com
Mchezaji wa  clabu ya Liverpool Mohammed salaah aibukaa kidedea baada ya kushinda tuzo ya BBC ya mchezaji bora afrika mwaka huu akiwabwaga wapinzani wake ambao walikuwa victor moses,aubameyang,mane na keita

Arsenal yaanza kupataa makombora ya Sweden europa league

     dulahots. blogspot. com
Arsenal imepangwa kucheza dhidi ya timu ya Ostersunds ya nchini Sweden katika Hatua ya 32 Bora ya michuano ya Europa League. 

Arsenal itawavaa wapinzani wao hao ambao wanafundishwa na Graham Potter ambaye ni raia wa Uingereza. 

Atletico Madrid wao wamepangwa kukutana na Copenhagen wakati Borussia Dortmund itakutana na wabishi kutoka Italia, Atalanta ambao waliifunga Everton nyumbani na ugenini katika hatua ya makundi ya michuano hiyo. 

Makocha wawili waliowahi kufanya kazi England wanatarajia kukutana pia katika hatua hiyo wakati ambapo Celtic inayonolewa na Brendan Rodgers itakutana na Zenit St Petersburg iliyochini ya Roberto Mancini. 

Kocha Gennaro Gattuso wa AC Milan ataiongoza timu yake hiyo kuivaaa Ludugorets ya Bulgaria. 

Ratiba kamili inaonyesha hatua hiyo itachezwa Februari 15 wakati mechi za marudio ni Februari 22, mwakani 2018. 

RATIBA KAMILI YA 32  
Borussia Dortmund vs Atalanta 

Nice vs Lokomotiv Moscow 

Copenhagen vs Atletico Madrid 

Spartak Moscow vs Athletic Bilbao 

AEK Athens vs Dynamo Kiev 

Celtic vs Zenit St Petersburg 

Napoli vs Leipzig 

Red Star Belgrade vs CSKA Moscow 

Lyon vs Villarreal 

Real Sociedad vs Salzbug 

Partizan Belgrade vs Viktoria Plzen 

Steaua Bucharest vs Lazio 

Ludogorets vs AC Milan 

Astana vs Sporting Lisbon 

Ostersunds vs Arsenal 

Marseille vs Braga 

Chelsea wataweza kuifunga Barcelona

      dulahots. blogspot. com
Shirikisho la soka barani Ulaya leo limefanya droo ya kupanga mechi za hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA ambapo Mabingwa watetezi Real Madrid wataanzia Bernabeu kuikaribisha Paris Saint-Germain PSG. 

Katika droo hiyo pia mabingwa wa England Chelsea, wataanzia nyumbani kuwakaribisha vinara wa La Liga FC Barcelona. Kikubwa katika mchezo huu ni mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi akiwa hajawahi kuifunga Chelsea katika mechi nane alizokutana na timu hiyo na kufanya Chelsea iwe ndio timu ambayo amecheza nayo mara nyingi zaidi bila kuifunga. 

Vinara wa EPL Mamchester City itaanzia ugenini dhidi ya FC Basel. Manchester United itakuwa ugenini kucheza na Sevilla ya Hispania. Mchezo mwingine utawahusisha wanafainali wa msimu uliopita Juventus ya Italia ambayo itaanzia nyumbani dhidi ya Tottenham. 

Mabingwa mara tano wa UEFA Liverpool itasafiri hadi Ureno kucheza na FC Porto. Bayern Munich itaanzia nyumbani kwenye dimba la Allienz Arena kucheza na Besiktas ya Uturuki. Shaktar Donetsk ya Uturuki itakuwa nyumbani kuanza na AS Roma. 

Neymar Jr anarejea kwa mara ya kwanza kwenye ardhi ya Hispania kikazi akiwa na PSG kuikabili Real Madrid. Msimu uliopita PSG iliondolewa na Barcelona kwa kufungwa jumla ya mabao 6-5 wakati huo Neymar akiwa na Barcelona.

Libya yaicharazaa Zanzibar heroes 1_0

dulahots. blogspot.com
ZANZIBAR imepoteza mchezo wake wa mwisho wa Kundi A Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kuchapwa 1-0 na Libya mchana wa leo Uwanja wa Jomo Kenyatta mjini Machakos, Kenya.  

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Abdoul Karim Twagirumukiza wa Rwanda aliyesaidiwa na Tigle Belachew wa Ethiopia na Herve Kakunze wa Burundi, bao pekee la Libya ambao ni waalikwa kutoka Kaskazini mwa Afrika, limefungwa na Alharaish Zakaria dakika ya 24 kwa shuti la mbali kutoa nje kidogo ya boksi. 

Zanzibar iliyopumzisha baadhi ya nyota wake kwa ajili ya mechi ya Nusu Fainali, ilijitahidi kusaka bao la kusawazisha, lakini bahati haikuwa yao leo. 

Pamoja na kipigo hicho, Zanzibar ya kocha Hemed Suleiman bado inaongoza Kundi A kwa pointi zake saba, kufuatia awali kushinda mechi mbili na sare moja. Libya inapanda hadi nafasi ya pili baada ya ushindi huo, ikifikisha pointi sita baada ya awali kutoa sare za 0-0 mara tatu. 

Wenyeji, Kenya wanahitaji kuifunga Tanzania Bara katika mchezo unaofutia hivi sasa ili kufikisha point inane na kuipiku Libya na kwe nda Nusu Fainali. 

Kikosi cha Zanzibar kilikuwa; Ahmed Ali Suleiman, Mohamed Othman Mmanga, Mwinyi Hajji Mngwali, Abdallah Haji Shaibu ‘Ninja’, Issa Haidari Dau, Abdul-Azizi Makame Hassan, Seif Abdalla Rashid, Abdul-Samad Kassim Ali, Khamis Mussa Makame, Amour Suleiman Muhamad na Adeyum Ahmed Seif/Mohammed Issa ‘Banka’ dk85. 

Libya; Azzaqah Ahmed, Eltribi Ahmed, Elbarasi Taher, Sabbou Motasem, Aleyat Mohamed, Madeen Muhanad, Shafshuf Suhib, Taktak Muftah, Alharaish Zakaria, Almaryami Khalid na Maetouq Ali.

Mourinhoo awapondaa man city

dulahots.blogspot.com
Kila mwanahabari duniani wakati wa mchezo mkubwa ambao unamhusu Jose Mourinho huwa wanamtafuta ili kufahamu nini maoni yake, ndio na Mourinho amekuwa bora kuwapa wanahabari kile wanachokitaka. 

Jose Mourinho amesema City hawakupaswa kushangilia kutokana na aina ya mabao ambayo wamefunga, huku akidai kwamba mabao yote mawili ya Manchester City yalionekana yalikuwa ya bahati tu. 

Mourinho amehoji kwamba kama Manchester City waliwashika sana kama watu wanavyodai mbona golikipa wao Ederson ndio golikipa aliyeokoa hatari zaidi (Shambulizi la Lukaku na Mata) kuliko golikipa wao. 

Mourinho amempongeza refa wa mchezo huo Michael Oliver kwa alivyokuwa mtulivu katika mchezo huo lakini akamponda kwa kuwanyima penati dakika za mwisho ambapo Ander Herrera alionekana akiangushwa katika eneo la 18. 

Manchester City sasa wanakuwa wamefikisha alama 46 baada ya mchezo wa jana zikiwa ni alama 11 mbele ya Manchester United jambo ambalo tayari linawapa nafasi kubwa kuwa mabingwa wa EPL msimu huu.

Motoo umewakaa unaambiwa UEF raundi ya 16

Shughulii imewakaaa raundi ya 16
dulahots.blogspot.com

Kocha boraa Mara nne mfululizoooo EPL gurdiola

         @dullahots.blogspot.com Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kutwaa tuzo ya kocha bo...