Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba SC, Shiza Kichuya anatarajiwa kurejea dimbani Jumapili hii kuwavaa Stand United katika mchezo wa mzunguko wa tano baada ya kupona majeraha aliyoyapata katika mechi iliyopita dhidi ya
Mbao FC.
Hayo yamewekwa wazi na Afisa wa Habari wa wekundu wa Msimbazi, Haji Manara ambaye amesema winga huyo mwenye msaada mkubwa katika kikosi hicho ameanza mazoezi mepesi tokea jana na wenzake.
"Hali ya kikosi cha Simba hadi sasa ni nzuri, tulikuwa na majeruhi mmoja Shiza Kichuya ambaye tayari ameshaanza mazoezi, kwa hiyo kama kocha ataamua kumtumia siku ya Jumapili atatumika, tunawaomba watu wa Kanda ya ziwa waje kuipa ushirikiano timu yao kama walivyo walivyofanya katika mechi dhidi ya Mbao FC", amesema Manara.
Simba SC inatarajiwa kushuka katika dimba la Kambarage Mkoani Shinyanga Oktoba mosi mwaka huu kuwavaa Stand United FC huku ikiwa nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi nane, wakati Stand United FC ipo nafasi ya 12 ikiwa na alama tatu.dulahots.blogspot.com
dulahots.blogspot.com ni blog inayokuhabarisha habari zote za kimichezo,burudani na magazeti Karibuni🙏👇
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kocha boraa Mara nne mfululizoooo EPL gurdiola
@dullahots.blogspot.com Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kutwaa tuzo ya kocha bo...
-
Msimbazi speedi ya 4G+ MSHAMBULIAJI Mganda, Emmanuel Arnold Okwi leo amefunga mabao mawili na kuseti mawili, Simba SC ikiibuka na us...
-
Kichupaa kipyaa toka wcb, rayvan ft Niki wa pili "SIRI" ni Nouma sanaaa Fanya kuicheki hapo chini @dullahots.blogspot.com
-
dulahots. blogspot.com ZANZIBAR imepoteza mchezo wake wa mwisho wa Kundi A Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Chall...


No comments:
Post a Comment