Powered By Blogger

28.9.17

Msemaji wa club ya simba sport haji manara amvaa chirwa

Afisa habari wa Klabu ya Simba Haji S Manara amelaani kitendo cha Shambulio lililofanywa na mchezaji wa klabu ya Yanga Obrey Chirwa la kumshambulia muandishi wa gazeti hapa nchini aliyekuwa akitekeleza wajibu wake. 

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram Manara amekitafsiri kitendo kilichofanywa na mchezaji Chirwa kama ushamba na kutaka kilaaniwe na watu wengi. 

"Huu ni ushamba!! tunapaswa kuulani wote, tuheshimu taaluma za watu, umaarufu wetu kinyesi tusiutumie vibaya" ameandika Manara. 

Chirwa anadaiwa kumshambulia Mwanahabari na Mpiga picha wa gazeti hapa nchini alipokuwa akimpiga picha wakati wakifanya mazoezi katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam hapo juzi. 

No comments:

Post a Comment

Kocha boraa Mara nne mfululizoooo EPL gurdiola

         @dullahots.blogspot.com Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kutwaa tuzo ya kocha bo...