Powered By Blogger

30.9.17

Kila mechi kwetu ni fainali Mbaraka Yusuph afunguka


Mshambuliaji tegemeo wa Azam FC, Mbaraka Yussuf

Mshambuliaji tegemeo wa Azam FC, Mbaraka Yussuf amesema kila mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara kwao ni kama fainalidulahots.blogspot.com. 

Mbaraka Yussuf amesema wanajua ya kuwa kila mchezo wanaocheza unakuwa mgumu kutokana na timu pinzani kuwakamia, lakini amedai malengo yao ni kushinda kila mtanange. 

“Kwanza namshukuru Mungu kucheza mechi hizi salama pia namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kufunga pia napenda sana kujitahidi kadiri ya uwezo wangu kila mechi niwe naweza kufunga ili niweze kuweka rekodi nzuri katika msimu huu na nawaahidi mashabiki kuwa mfungaji bora” amesema Mbaraka Yussuf 

Akizungumzia kuhusu mchezo ujao dhidi ya Singida United, Mbaraka amesema: 

“Kwa kweli mechi yoyote ile Azam ikikutana na timu yoyote mechi inakuwa ngumu kwa vile watu wanakuwa wanakamia sana, kauli mbiu yetu kila mechi sisi kwetu ni fainali na tunapambana ili tuweze kufunga. ” amesema.

No comments:

Post a Comment

Kocha boraa Mara nne mfululizoooo EPL gurdiola

         @dullahots.blogspot.com Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kutwaa tuzo ya kocha bo...