KIKOSI CHA YANGA.
Katibu Mkuu wa chama hicho, Athumani Kilundumya,. Alisema kuwa wanaamini mchezo huo wa kirafiki utaleta changamoto kwa mkoa wao ambao hauna timu inayoshiriki ligi kuu msimu huu.
“Tupo kwenye mazungumzo na uongozi wa Yanga na tunaamini ndani ya muda mfupi kuanzia sasa tutakuwa tumepata jibu,” alisema Kilundumya.
Alisema mara baada ya kupata majibu watafanya utaratibu na kuangalia Mabingwa hao wa soka nchini wacheze na timu ipi ya mkoani hapo.
Wiki iliyopita, Simba ambayo ipo mkoani Shinyanga ikijiandaa kucheza mchezo wa ligi kuu kesho dhidi ya Stand United, ilicheza mchezo wa kirafiki na Milambo ya Tabora katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi na timu hizo kutoka bila kufungana.
Yanga inatarajia kwenda kanda ya ziwa baadae mwezi ujao kucheza na Kagera Sugar mjini Bukoba (Oktoba 14) na baadae kucheza na Stand United mkoani Shinyanga (Oktoba 22).
Tarefa inataka kutumia safari hiyo ya Yanga kanda ya ziwa kupata mchezo wa kirafiki kama walivyofanya kwa Simba ambayo ilianza kucheza na Mbao FC jijini Mwanza kabla ya kuelekea Shinyanga.
No comments:
Post a Comment